IQNA

Morocco yatoa wito wa mapambano dhidi ya propaganda chafu zinazoulenga Uislamu

13:37 - October 13, 2010
Habari ID: 2012089
Katibu wa Wizara ya Mawasilino ya Morocco Ridhwan Balarabi ameitaka Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kuchukua hatua za kimsingi za kupambana na propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya dini ya Kiislamu.
Ridhwan Balarabi aliyasema hayo jana katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Habari na Masuala ya Kiutamaduni ya jumuiya ya OIC na kuongeza kuwa kuna udharura kwa kamati hiyo kufanya juhudi kubwa za kuarifisha sura halisi ya Uislamu kama dini ya amani, kuvumiliana na upendo na kupambana na propaganda zinazoichafulia jina dini hiyo kote duniani.
Amepongeza kazi za kamati hiyo katika nyanja za mawasiliano na dini nyingine na kupanua utamaduni wa mazungumzo kati ya dini tofauti na akaongeza kuwa kamati hiyo inapaswa kufanya jitihada kubwa zaidi za kukabiliana na hujuma za maadui wa Uislamu na Waislamu.
Katibu wa Wiara ya Mawasiliano ya Morocco ameashiria juhudi zinazofanywa na Kamati ya Quds Tukufu kwa ajili ya kulinda utambulisho wa Kiislamu wa Quds na akasema anafurahishwa mno kuona kadhia ya Quds na Palestina inapewa umuhimu katika Kamati ya Kudumu ya Utamaduni ya OIC. Harun Yahya amezitaka pia nchi za Kiislamu kutilia maanani zaidi vyombo vya habari na kuanzisha redio na televisheni zaidi na kuimarisha ushirikiano wa kihabari kwa lengo la kuimarisha umoja wa Waislamu na kukabiliana na hujuma za maadui. 674268

captcha