IQNA

Mashindano ya pili ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu kufanyika Iraq

12:48 - October 14, 2010
Habari ID: 2012667
Awamu ya pili ya mashindano ya kitaifa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Iraq yatafanyika tarehe 23 hadi 25 Oktoba huko Bagdad, mji mkuu wa Iraq.
Akitangaza habari hiyo, Ra'd Adnaan, Mkurugenzi wa Darul Qur'an al-Karim ya mjini Nasiriyyah, amesema kuwa mashindano hayo yameandaliwa na Kamati Kuu ya Kudumu ya Qur'ani Tukufu ambayo inafungamana na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri la Iraq na kwamba yatafanyika katika hatua mbili za kusoma na kuhifadhi Qur'ani.
Makari 54 na mahafidhi 81 wa Qur'ani Tukufu kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq wanashiriki katika mashindano hayo.
Bwana Adnaan amesema kuwa mashindano hayo ndiyo mashindano makubwa na muhimu zaidi ya Qur'ani nchini Iraq. 674439
captcha