Mwanafikra huyo alipatwa na mshtuko wa ubongo na kuaga dunia mara tu baada ya kufikishwa katika hospitali moja ya mjini al-Mubarriz. Alizikwa jana Jumatano ya jana. B
aada ya kupata masomo yake ya msingi katika mji huo mwanafikra huyo mashuhuri wa Kiislamu alipata elimu ya juu ya kidini katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbalaa.
Swalih Muhammad as-Sultan aliyezaliwa mwaka 1924 alipata masomo yake kutoka kwa walimu mashuhuri wa wakati huo wa Iraq wakiwemo marehemu Seyyid Muhsin Hakim na Sayyid Abul Qassim Khui. 674774