IQNA

Kanali ya televisheni ya ‘Ahlul Qur'an’ yaanzishwa

9:58 - October 17, 2010
Habari ID: 2013873
Kanali ya Televisheni ya Satalaiti ya 'Ahlul Qur'an' imeanzishwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Kanali hiyo ya lugha ya Kiarabu imeazishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu na kuhudumia kitabu hicho kitakatifu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu, kanali hiyo imeanzishwa hivi karibuni na kwamba itajitahidi kutangaza juhudi za nchi za Kiislamu katika uga wa mafunzo na uzingatiwaji Qur'ani Tukufu.
Aidha kanali hiyo italenga kuwahimiza watu wajifunze Qur'ani Tukufu na kutekeleza mafunzo yake mbali na kuinua hadhi ya wanaohifadhi Qur'ani tukufu katika jamii za Kiislamu.
Kanali hiyo ya televisheni inapatikana katika sataliti ya Arabsat katika frikuensi ya 12054 V.

676155
captcha