IQNA

Swala ya Ijumaa ya Waislamu mbele ya jumba la Congress ya Marekani

10:05 - October 17, 2010
Habari ID: 2013984
Ijumaa iliyopita Waislamu wanaoishi katika mji wa Washington waliswali mbele ya Congress ya Marekani ikiwa ni katika hatua yao ya kulalamikia ubaguzi wanaofanyiwa Waislamu nchini humo.
Umati wa watu wapatao 600 uliswali swala ya Ijumaa katika eneo la magharibi la jumba la Congerss ya Marekani kwa lengo la kulalamikia ubaguzi na hujuma iliyopangwa inayoendeshwa katika baadhi ya miji ya Marekani dhidi ya itikadi za Waislamu.
Wamemtaka Rais Barack Obama aingilie kati mara moja na kuwafanyia uadilifu raia wa Marekani wasiokuwa Wakristo.
Vilevile Waislamu waliokusanyika katika eneo hilo wametaka chuki inayoendeshwa nchini Marekani dhidi ya Uislamu ikomeshwe mara moja. 675759
captcha