Sherehe ya kubadilishwa pazia hilo itahudhuriwa na viongozi wa kieneo wa Saudi Arabia, mabalozi na wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu.
Swalih al-Hasin, mkuu anayesimamia masuala ya misikiti miwili mitakatifu ya Masjidul Haram na Masjid an-Nabii (saw) anatazamiwa kumkabidhi Abdul Aziz al-Sheibi anayesimamia shughuli ya pazia la al-Kaaba pazia jipya la msikiti huo hapo tarehe Mosi Dhil Hijja.
Pazia hilo lililogharimu riali milioni 20 za Saudi Arabia limetengenezwa katika kiwanda kimoja cha nchi hiyo na lina urefu wa mita 14 kwenda juu na upana wa mita 47.
Katika thuluthi moja ya juu ya pazia hilo kuna utepe wenye upana wa sentimita 95 uliorembwa kwa aya za Qur'ani Tukufu.
Pazia hilo ambalo limefumwa kwa hariri halisi litabadilishwa na lile la zamani baada ya kuoshwa kwa maji ya manukato kutoka eneo la Kashan nchini Iran. 676551