IQNA

Kongamano la Muujiza wa Qur'ani laanza mjini Madina

16:35 - October 18, 2010
Habari ID: 2015311
Kongamano la Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani na Suna za Mtume (saw) limeanza katika mji mtakatifu wa Madina likihudhuriwa na wanaharakati wa kike wa masuala ya Qur'ani.
Kongamano hilo linafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Rimas mjini Madina likihudhuriwa na wanaharakati wa kike kutoka maeneo mbalimbali ya Saudi Arabia, shakhsia mbalimbali wa kielimu na wasomi wa vyuo vikuu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Jumuiya ya Muujiza wa kisayansi wa Qur'ani ya mjini Madina Balqis Sharif Nasir amesema katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwamba kubainisha miujiza ya kisayansi ya Qur'ani na suna za Mtume ni miongoni mwa nyenzo muhimu za kulingania dini ya Kiislamu katika zama hizi.
Amesema kuwa ujumbe wa kongamano hilo ni kubainisha hakika za miujiza ya kisayansi ya Qur'ani na suna kwa mujibu wa vigezo vya sheria na kutumia miujiza hiyo katika ulinganiaji wa dini ya Mwenyezi Mungu.
Fatima Mujahid mwenyekiti wa kitengo cha wasichana cha jumuiya hiyo pia alitoa hotuba katika kongamano hilo akisema kuwa miongoni mwa malengo ya kikao hicho ni kueleza umuhimu wa miujiza ya kisayansi ya Qur'ani, kuimarisha misingi ya itikadi na moyo wa kuwajibika kati ya wanawake na kuzidisha mapenzi ya Qur'ani na suna za Mtume (saw).
Makala mbalimbali zimewasilishwa na wasomi wa kike wa Saudi Arabia katika kongamano hilo. 677455


captcha