IQNA

Uturuki yatetea ufunguzi wa Msikiti pekee mjini Athens

9:35 - October 19, 2010
Habari ID: 2015457
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan mwenye misimamo ya Kiislamu anatazamiwa kutembelea mji mkuu wa Ugiriki Athens ambapo pia atazuru msikiti wa Fatihiya ambao ni msikiti wa pekee mjini humo. Erdoğan atajaribu kuwashawishi wakuu wa mji huo kuruhusu msikitu huo unaokaribia kuporomoka ukarabatiwe.
Kwa mujibu wa gazeti la Milliyet la Uturuki, kwa miaka mingi sasa kumekuwepo mjadala katika duru za kisiasa na kidini nchini Ugiriki kuhusu ukarabati wa Msikiti mjini Athens.
Katika safari yake mjini Athens tarehe 22 Oktoba, Erdoğan atautembelea Msikiti wa Fatihiya uliojengwa katika zama za Uthmaniya na ambao sasa unakaribia kubomoka huku serikali ya Ugiriki ikiwazuia Waislamu kuutumia. Athens ndio mji mkuu pekee wa nchi za Ulaya ambayo hauna Msikiti. Kuna karibu Waislamu laki mbili katika mji huo lakini hadi sasa hawana sehemu maalumu ya ibada.
Msikiti wa Fatihiya ulijengwa mwaka 1456 Miladia kufuatia amri ya Fath Sultan Mohammad.
Msikiti huo ndio athari pekee iliyobakia kutoka zama za Utawala wa Ukhalifa wa Uthmaniya huko Athens. Msikiti huo ulifungwa mwaka 1829 na hadi leo haujafunguliwa tena.
captcha