IQNA

Moscow, mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu

10:41 - October 19, 2010
Habari ID: 2015638
Mashindano ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu ya Russia yanatazamiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba katika mji wa Moscow.
Mashindano hayo yatasimamiwa na Baraza la Mamufti wa Russia likishirikiana na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Baraza la Mamufti wa Russia limewaalika wasomaji kutoka nchi kadhaa kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano hayo ya kimataifa.
Inatazamiwa kuwa wawakilishi wa nchi 30 watashiriki katika mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani ya Russia.
Kandokando ya mashindano hayo kutafanyika maonyesho ya sanaa na ratiba za kasida za makundi kutoka Jamhuri ya Tatarstan na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mashindano ya kusoma Qur'ani ya Russia yamekuwa yakifanyika tangu miongo kadhaa iliyopita na yanahesabiwa kuwa ni sehemu ya shughuli za kiutamaduni za nchi hiyo. Mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuielimisha jamii utamaduni na ada za dini tukufu ya Kiislamu. 678133

captcha