Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, Hussein Baharvand, mtafiti mashuhuri wa seli shina katika Taasisi ya Utafiti ya Royan ametunukiwa zawadi ya kwanza ya elimu ya biolojia ya ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2010.
Katika hafla ya kutunukiwa zawadi hiyo Mirsadov Ulmas msomi mwingine wa Tajikistan alitunukiwa tuzo ya kemia ya ulimwengu wa Kiislamu. Wasomi wengine waliotunukiwa zawadi katika hafla hiyo ni Muhammad Qassim Jan wa Pakista, Ubeidat Zeid wa Jordan, Muhammad Shibbat wa Palestina na Muhammad Amin Imbi wa Malaysia walitotunukiwa zawadi za Kemia, hesabati, fizikia na teknolojia katika Ulimwengu wa Kiislamu kwa utaratibu huo.
Kuimarisha kiwango cha elimu na teknolojia katika nchi za Kiislamu ndilo lengo muhimu la kufanyika kikao hicho cha tano mjini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia.
Kikao hicho kimeanza leo Jumanne kwa hutuba ya Waziri wa Elimu wa Malaysia pamoja na Mahathir Muhammad Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo ambaye pia ni mjumbe wa ISESCO anayeshughulikia masuala ya kuimarisha mazungumzo baina ya tamaduni na staarabu mbalimbali. 678604