Akibainisha suala hilo, Ayashur amesema kuwa watu wasiojulikana walivunja lango la msikiti huo karibu saa kumi alfajiri na kutupa mada za moto katika ukumbi wa kuiingia kwenye msikiti huo ulio na uwezo wa kubeba watu 800. Baraza hilo la Waislamu limelaani vikali kitendo hicho cha kinyama na kuwataka wakazi wa Alsace kuheshimu na kulinda umoja wa kitaifa pamoja na kukabiliana vilivyo na vitendo kama hivyo vya ubaguzi wa rangi. Mkuu anayesimamia msikiti huo ambao ni wa Waturuki wanaoishi nchini Ufaransa amelaani kitendo hicho na kusema kuwa licha ya kuwa msikiti huo umezungukwa na kamera za udhibiti lakini sura za washambuliaji hao hazikuweza kunaswa vyema kutokana na giza lililokuwepo wakati wa kufanyika hujuma hiyo. Amesema habari ya hujuma hiyo tayari imetolewa kwa polisi na kuelezea matumaini yake kwamba watafanya kila liwezekanalo ili kuwatia nguvuni wahalifu waliohusika na kitendo hicho cha jinai. Amewataka Waislamu kukabiliana kwa utulivu na kitendo hicho cha kichochezi. 678151