IQNA

Matangazo ya televisheni ya Ahlul Bait yasimamishwa Nilesat

19:22 - October 20, 2010
Habari ID: 2016843
Matangazo ya kanali ya televisheni ya Ahlul Bait ya Waislamu wa madhehebu ya Shia yamesimamishwa katika satalaiti ya Nilesat ya Misri.
Wizara ya Habari ya Misri imechukua hatua hiyo katika harakati za kupiga vita madhehebu ya Shia na kuwawekea mashinikizo zaidi Waislamu wa madhehebu hiyo na vilevile jitihada za kuzuia kasi ya kueneza mafundisho ya Ahlul Baiti wa Mtume katika nchi za Kiarabu.
Waziri wa Habari wa Misri Anas al Faqqi amedai kuwa matangazo ya televisheni ya Ahlul Bait yamesimamishwa kwa muda kutokana na kile alichokiita ni kuzusha vitina za kimadhehebu, kuvunjia heshima itikadi za wafuasi wa dini na madhehebu nyingine na kutangaza uzushi!
Hii ni katika hali ambayo matangazo ya kanali hiyo ya televisheni ya Ahlul Bait yenye makao yake nchini Iraq, yamekuwa yakitetea mafundisho ya madhehebu ya Ahlul Baiti wa Mtume (saw) na Shia na kujibu maswali na uzushi unaotolewa na Mawahabi dhidi ya wafuasi wa madhehebu hiyo. Kanali hiyo ya televisheni haijawahi kutangaza vipindi vinavyokebehi au kufunjia heshima itikadi za madhehebu au dini nyingine.
Wizara ya Habari ya Misri imezitahadharisha pia televisheni nyingine za Waislamu wa Kishia zinazorusha matangazo yao kupitia satalaiti ya Nilesat kama kanali ya al Anwar na kutishia kusimamisha matangazo yao.
Hatua hiyo ya serikali ya Misri inachukuliwa katika hali ambayo Sheikh Mkuu wa al Azhar ambacho ndicho kituo kikubwa zaidi na marejeo ya juu ya Waislamu wa madhehebu ya Suni Ahmad al Tayyib amekuwa akifanya jitihada kubwa za kuondoa dhulma na manyanyaso yanayowapata Waislamu wa madhehebu ya Shia Ja'fariyya nchini humo na katika nchi nyingine za Kiarabu. 679043
captcha