Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika kitengo cha kimataifa cha maonyesho hayo, mtaalamu wa grafiki ya kompyuta, Ali Njoroge kutoka Kenya amepata tunzo kutokana na kazi zake stadi za kisanaa na kiutamaduni.
Katika kitengo cha uuzaji wa programu za kompyuta, Ibrahim Bahadori kutoka Iran amepata tunzo kutokana na kazi zake asili za Kiirani na Kiislamu za kiutamaduni.
Sherehe za kuzawadiwa wataalamu hao zimehudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Sayyed Mohammad Husseini na maafisa wengine wa utamaduni.
679256