Kwa mujibu wa tovuti ya RTB mashindano hayo yamefanyika katika makundi tofauti ya wanawake na wanaume wanaofanya kazi katika wizara hiyo ambapo washindi wanne wa kwanza katika kila kundi walichaguliwa kushiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano.
Katika hatua hiyo iliyofanyika wiki hii, washindi watatu tokea wa kwanza hadi wa tatu walitangazwa kuwa washindi wa mwisho na kutunukiwa zawadi kutokana na juhudi walizofanya katika mashindano hayo.
Zawadi ya washindi wa kwanza katika makundi mawili hayo ilikuwa ni tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi kutoka hija ya mwaka huu, ambayo ilikabidhiwa kwa washindi na Naibu Waziri wa Elimu na Malezi wa Brunei. 679953