Shirika la Habari la Ufaransa limeripoti kuwa kasisi huyo wa Lebanon ambaye alikuwa akizungumza katika Baraza la Makasisi wa Mashariki ya Kati tena mbele ya Papa Benedict wa 16 amedai kuwa sababu ya kuenea Uislamu na Qur'ani na kupata ushawishi duniani ni tabia ya Waislamu ya kutumia mabavu na ukatili.
Baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Makasisi hao kasisi huyo wa Lebanon ametoa taarifa akidai kuwa Qur'ani Tukufu inaficha hakika za ulimwengu wa Kikristo na inawaruhusu Waislamu kuwaua wasiokuwa Waislamu hususan Wakristo! Amedai kuwa dini ya Kiislamu haiwapi wafuasi wake na wafuasi wa dini nyingine uhuru wa kidini.
Matamshi ya kasisi huyo yametolewa katika hali ambayo makasisi wenzake waliohudhuria kikao hicho wamesisitiza juu ya udharura wa kuwepo mazungumzo kati ya Uislamu na Ukristo. 680364