Kongamano hilo la kimataifa linasimamiwa na Shirika la Sayansi, Utamaduni na Elimu la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO likishirikiana na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani na Baraza la Kiislamu la Croatia.
Kongamano hilo linafanyika kwa lengo la kuwaenzi mahafidhi wa Qur'ani, kuwaarifisha kwa walimwengu, kupanua elimu na maarifa yao na kadhalika.
Kongamano hilo pia linajadili jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa katika kufunza Qur'ani, mbinu za kuhifadhi Qur'ani na jinsi ya kuboresha mbinu hizo. 680314