Mashindano hayo yalifanyika kwa usimamizi wa Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Hamza nchini Ethiopia kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yamefanyika katika daraja tano za kuhifadhi Qur'ani kamili, juzuu 20, juzuu 15, juzuu 10 na juzuu 5 za Qur'ani Tukufu.
Maafisa na viongozi wa jumuiya mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya Qur'ani za Ethiopia wamehudhuria sherehe ya kuwazawadia washindi wa mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Masuala ya Dini na Utamaduni ya al Ihsan ya Ethiopia ametoa hotuba katika sherehe hiyo akisisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika mashindano ya Qur'ani Tukufu katika kueneza utamaduni wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na ameishukuru Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani kwa kufanikisha mashindano hayo.
680604