Wataalamu hao wa haki za binadamu wanatoka nchi za Malaysia, Palestina, Senegal na Saudi Arabia na wanachunguza na kubadilishana mawazo kuhusu njia za kukomesha mateso na mzingiro wa Israel dhidi ya raia wa Gaza.
Mkutano huo unasimamiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC. Timu hiyo ya wanasheria inakusudia kutekeleza maamuzi yaliyochukuliwa mwaka jana na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama katika jumuiya ya OIC.
Wanasheria hao wa Kiislamu pia wanachunguza suala la mashambulizi yaliyofanywa mapema mwaka huu na jeshi la utawala katili wa Israel dhidi ya msafara wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza. 681131