Katika ujumbe aliomtumia Sheikh al-Azhar, Ayatullah Sub'hani amemwambia kwamba amefurahishwa na msimamo wake wa kuyajali madhehebu yote ya Kiislamu, ikiwemo ya Shia Imamiyyah. Amesema, mashekhe na wanazuoni wengine muhimu waliomtangulia Sheikh Tayyib akiwemo Ayyatullah Allama Sayyid Hussein Burujerdi wa Iran na Sheikh Mahmoud Shaltut wa Misri pia walisisitiza sana umoja na mshikamano wa Waislamu.
Ayatullah Subhani amesema kuwa katika kipindi hiki nyeti kwa umma wa Kiislamu ambapo maadui wa Uslamu wanafanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuwasha moto wa fitina na hitilafu miongoi mwa Waislamu kupitia vyombo vyao vya habari na kipropaganda, Waislamu wema na walinganiaji wa fikra ya kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu wanapasa kutekeleza vyema majukumu yao katika kivuli cha imani ya Mwenyezi Mungu mmoja, Qur'ani na Mtume Mtukufu (saw). 681464