IQNA

Kikao cha kamati ya utendaji ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu chaanza Imarati

12:12 - October 25, 2010
Habari ID: 2019137
Kikao cha Kamati ya Utendaji ya mkutano wa 24 wa Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu kilianza jana Jumapili huko Abu Dhabi, mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kikao hicho kinafanyika chini ya uenyekiti wa Abdul Aziz Abdalla al-Ghureir, Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Imarati.
Uchunguzi wa mapendekezo yaliyotolewa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kuhusiana na kurekebishwa katiba na ustawi wa kiufundi wa sekretarieti ya Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu ni moja ya masuala muhimu yatakayojadiliwa katika kikao hicho. Al-Ghureir amesema kuwa kikao hicho kimefanyika kwa madhumuni ya kutafuta njia bora zaidi za kupambana na vitisho pamoja na changamoto kadhaa zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu. Amesema kuna udharura mkubwa wa kuwasilishwa mapendekezo ya kielimu ya kamati hiyo kwa kikao cha Muungano wa Mabunge ya Kiislamu kwa ajili ya kuchukuliwa uamuzi wa dharura wa kusimamisha haraka hatua zisizo za kisheria za utawala haramu wa Isreal za kubadili muundo wa kijamii wa Quds Tukufu huko Palesina inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu. 681486
captcha