Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bw.Muhammad Baqer Khorramshad ameyasema hayo Jumapili katika hafla ya kumuarifisha kama Mkuu mpya wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu. Ameongeza kuwa, leo katika uga wa kimataifa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatambuliwa kama nchi yenye nguvu kubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na Magharibi mwa Asia kwa mtazamo wa kisiasa na kiuchumi. Amesema kwa tazamo wa kiutamaduni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inahesabiwa kuma nguvu ya kimataifa.
Amesema kwa kuzingatia hayo, Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu lina jukumu muhimu kama mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimataifa.
Hafla ya kumuarifisha Bw.Muhammad Baqer Khorramshad kama Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu imehudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozi ya Kiislamu aliyemteua kuchukua wadhifa huo.
Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Mambo ya Nje Manoucher Mottaki na Hujjatul Islam wa Muslimin Muhammadi Golpayegani Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kati ya wengine.
Aliye kuwa Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu kabla ya Khorramshad, Bw.Mehdi Mostafavi sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na vile vile Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Nje.
681670