Kongamano hilo linasimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Muujiza wa Qur'ani na linajumuisha maonyesho ya miujuza ya kisayansi ya Qur'ani na suna za Mtume (saw).
Mkurugenzi wa ofisi ya Jumuiya Kimataifa ya Muujiza wa Qur'ani katika mji wa Jazan Abdur Rahman bin Ahmad Alush amesema kuwa kongamano hilo linahudhuriwa na watafiti wa masuala ya Qur'ani na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Saudi Arabia.
Ameongeza kuwa makala mbalimbali zinazojadili miujiza ya kisayansi ya Qur'ani, siri za tiba katika mtazamo wa Qur'ani, muujiza wa Qur'ani Tukufu na suna za Mtume kuhusu maji na Qur'ani, tafsiri ya dunia zimewasilishwa katika kongamano hilo. 682182