Kwa mujibu wa gazeti la Imarati la Al Bayan, katika taarifa hiyo iliyotolewa baada ya kumalizika kikao cha kamati ya utendaji ya Jumuiya ya Mabunge ya Nchi za Kiislamu huko Abu Dhabi, nchi za Kiislamu zimelaani vikali aina yoyote ya kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.
Taarifa hiyo imesema kuwa, 'mapambano ya mataifa dhidi ya ukaliaji mabavu wa kigene na jitihada za kupigania uhuru ni mambo ambayo hayawezi kuhusishwa na ugaidi hata kidogo'.
Jumuiya ya Mabunge ya Nchi za Kiislamu imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kukabiliana na misimamo ya kidini inayofurutu mipaka na kuimarisha ushirikiano wa wafuasi wa dini mbalimbali duniani.
682265