Sherehe hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Tun Razak na mkewe Rasma Mansur.
Bi Rasma Mansor amesema katika sherehe hiyo kwamba Waislamu wanawajibuka kupanua maarifa yao kuhusu dini hiyo tukufu na kuimarisha zaidi moyo wa umma wa Kiislamu.
Ameashiria kuwa suala la kuunda umma mmoja wa Kiislamu ni katika kutii amri ya Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa mashindano hao yaliyowashirikisha washindani 97 yalikuwa fursa nzuri kwa Waislamu wapya kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu dini ya Kiislamu na thamani za dini hiyo.
Mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia amesisitiza juu ya umuhimu wa kuundwa umma mmoja wa Kiislamu na akasema kuwa falsafa ya kuwepo umma huo ni pana zaidi na imevuka mipaka ya kaumu na ya kisiasa.
Rasma Mansur pia amezitaja jumuiya mbalimbali za Malaysia kusaidia mashindano ya Qur'ani Tukufu na ratiba zinazofanyika kwa shabaha ya kutukuza turathi na thamani za Kiislamu. 682853