Kikao hicho kitaendelea kwa muda wa siku nne. Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, kikao hicho kilichoandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait, kitaendeshwa chini ya uenyekiti wa Rashid al-Hammad, Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait anayeshughulikia Masuala ya Sheria na mbaye pia ni Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait.
Kikao hicho kitajadili masuala mbalimbali ya Kiislamu yakiwemo ya hukumu za kisheria, utekelezaji sheria, usimamizi wa makadhi kwenye mahakama, makadhi katika medani ya kazi na shughuli, jamii za Waislamu walio wachache na uchaguzi wa makadhi wa Kiislamu.
Wizara iliyotajwa ya Kuwait imesema lengo la kuandaliwa kikao hicho ni kujaribu kuziepusha baadhi ya jamii na fikra za kupindukia mipaka na ugaidi na wakati huohuo kuimarisha fikra wastani ulimwenguni. 683192