IQNA

Maonyesho ya Milan yanaakisi sura halisi ya Uislamu

11:40 - October 27, 2010
Habari ID: 2020679
Sheikh Duej Ibrahim as-Swabah, balozi wa Kuwait nchini Italia amesema kuwa kufanyika maonyesho ya kimataifa ya sanaa ya Kiislamu katika mji wa Milan ni jambo linaloandaa uwanja wa kuwasilishwa na kudhihirishwa sura halisi ya Uislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, Sheikh as-Swabah amesema maonyesho hayo yaliyoandaliwa na nchi yake huko Milan yanaonyesha athari za Kiislamu katika karne tofauti na hivyo kutoa fursa ya kufahamika vyema utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu katika karne hizo.
Amesema kuandaliwa maonyesa kama hayo kunaimarisha muono na ufahamu wa watu kuhusiana na Uislamu na wakati huohuo kuboresha uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na za Ulaya.
Maonyesho hayo yaliyoanza siku ya Jumanne Oktoba 19 yanaonyesha athari na vitu 300 vya kihistoria katika tawala tofauti za Kiislamu. Lengo ni kuzionyesha nchi za Magharibi thamani za utamaduni wa Kiislamu.
Maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi kwa wageni kutoka pembe tofauti za dunia kuyatembelea tarehe 31 Januari na kisha kuhamishiwa nchini Austria tokea tarehe 21 mwezi Machi mwakani. 683187
captcha