Ripoti hiyo imesema kuwa licha ya kushika kasi propaganda za kuwatisha watu kuhusu dini ya Kiislamu barani Ulaya (Islamophobia), lakini idadi ya watu wanaoingia kwenye dini hiyo pia imeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Ripoti ya YouGov imeendelea kusema kuwa: "Kati ya dini zote duniani, kasi ya kueneza Uislamu miongoni mwa watu inashika nafasi ya kwanza." Imesema wanawake mashuhuri wa Ulaya wanaonyesha hamu kubwa zaidi ya kuingia kwenye dini hiyo ya Mwenyezi Mungu kutokana na kuwa na uhusiano wa karibu na duru za Kiislamu na uwezekano wa kuwa pamoja na wafuasi wa dini hiyo.
Ripoti hiyo imesema kuwa watu wengi walioingia katika dini ya Kiislamu wanajihisi kuwa na utulivu zaidi wa kiroho wa kutekeleza wajibu wao wa kidini na wanafanya jitihada za kutekeleza faradhi zao za kidini kwa njia bora zaidi. Watu hao hujibu na kuonyesha radiamali haraka dhidi ya ubaguzi wa kimbari na vitendo vya kuuvunjia heshima Uislamu na hufanya juhudi za kutetea dini hiyo.
Mwanamke mashuhuri wa Ulaya aliyekubali na kuingia katika dini ya Kiislamu katika siku za hivi karibuni ni shemeji yake Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, Bibi Lauren Booth. Bi Booth ambaye ana mri wa miaka 43 alisilimu na kukubali dini tukufu ya Kiislamu baada ya kuzuru haram ya Bibi Fatima Maasuma amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran. 683528