IQNA

Kongamano la Tiba ya Kiislamu laanza Istanbul

15:25 - October 27, 2010
Habari ID: 2020981
Kongamano la tano la Jumuiya ya Kimataifa ya Historia ya Tiba ya Kiislamu limeanza katika Chuo Kikuu cha Istanbul nchini Uturuki.
Naibu Katibu wa kongamano hilo Nil Sari amesema katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwamba lengo lake kuu ni kusaidia utafiti unaofanyika katika nyanja za tiba ya Kiislamu.
Sari ameongeza kuwa kuna maandiko mengi ya kale kuhusu tiba ya Kiislamu katika nchi mbalimbali dunia lakini hadi sasa hakujafanyika jitihada za kukusanya pamoja na kushughulikia maandiko hayo. Amesisitiza kuwa moja ya kazi za kongamano hilo ni kuarifisha maeneo nyaraka hizo zinakopatikana na jinsi ya kuzikusanya.
Kongamano hilo linakamilisha shughuli zake kesho Alkhamisi. 683496
captcha