Kwa mujibu wa Taasisi wa Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, Bw. Ahmadi pia amependekeza kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Moustafa cha Iran ambacho kina matawi katika maeneo kadhaa ya dunia pia kifungue tawi nchini Afrika Kusini.
Pendekezo hilo pia limekaribishwa na Bw. Yusuf Dadu ambaye ameahidi kushirikiana katika kuanzisha chuo hicho nchini Afrika Kusini.
Akiashiria hatua ya kuvunjiwa heshima Qurani tukufu na njama za Uzayuni wa Kimataifa dhidi ya ubinaadamu na itikadi za Kiislamu, Yusuf Dadu amesema lazima kuwepo mikakati ya kuarifisha Qur'ani Tukufu katika jamii zisizo za Kiislamu.
682188