Masomo hayo yataendelea kwa kipindi cha miezi mitatu.
Masomo hayo yatahudhuriwa na watu 108 na yatawashirikisha vijana na watu wazima katika mji wa al Wakra nchini Qatar.
Taasisi ya masuala ya kheri ya Iddi bin Muhammad Al Thani imetangaza kuwa pambizoni mwa masomo hayo kutakuwa na ratiba za kidini, kiutamaduni na mafunzo ya sanaa.
Taarifa ya taasisi hiyo imesema kuwa lengo la masomo hayo ni kuwahamasisha wanawake na wasichana kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na kitabu cha Mwenyezi Mungu. 684597