IQNA

Kongamano la Kimataifa la Masoko ya Kiislamu kufanyika Dubai

11:37 - October 31, 2010
Habari ID: 2022257
Kongamano la Kimataifa la Masoko ya Kiislamu kitafanyika Machi 19 mwakani katika mji wa Dubai.
Kwa mujibu wa tovuti ya Emerald Insight, kongamano hilo linaandaliwa na Kitivo cha Uchumi na Elimu ya Soko katika Chuo Kikuu cha Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ushirikiano wa Shirika la Uchapishaji la Emerald la Uingereza.
Watakaoshiriki katika kongamano hilo ni wakurugenzi wa mashirika, maafisa wa serikali na washikadai katika sekta ya masoko kutoka nchi kadhaa duniani.
Kongamano hilo la siku tatu litajadili mada kama vile masoko ya Kiislamu, biashara ya Kiislamu, watumiaji wa bidhaa Waislamu, matangazo ya biashara ya bidhaa za Kiislamu, maadili katika masoko ya Kiislamu, masoko ya bidhaa halali, uuzaji huduma za kifedha za Kiislamu, soko la intaneti la Kiislamu, sekta ya mavazi ya Kiislamu, sekta za bidhaa za afya. Mada nyinginezo zitakazojadili katika kikao hicho ni pamoja na uhasibu na uchumi wa Kiislamu na uedeshaji wa Kiislamu.
Wanaotaka kushiriki katika kongamano hilo wanaweza kutuma makala zao kwa njia ya barua pepe ifuatayo kabla ya tarehe 20 Januari 2011 islamicmarketing2011@emeraldinsight.com
Makala bora zaidi za kongamano hilo zitachapishwa katika Jarida la Kiislamu la Journal of Islamic Marketing. 685170
captcha