Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Yemen kikao hicho kilifanyika katika mji wa Tarim nchini humo kuanzia 3-5 Oktoba na kuhuduriwa na maulamaa, taasisi na mashirika ya Kiislamu pamoja na maafisa wa serikali ya Yemen.
Katika taarifa yao washiriki wa kongamano hilo walitoa wito kwa mashirika na taasisi za Kiislamu duniani kujihusisha katika mikakati ya mwamko wa Kiislamu duniani na vile vile kuinua hadhi ya maulamaa na wasomi wa Kiislamu ambao wanatambuliwa kama warithi wa Mitume. Kongamano hilo liliandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Yemen. 684912