Kikao hicho kilifanyika pambizoni mwa maonyesho ya kimataifa ya magazeti na mashirika ya habari yanayoendelea mjini Tehran.
Sayyid Muhammad Hussein, Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu, Maryam Mujtahidzadeh, Mshauri wa Rais wa Iran na pia Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Wanawake na Familia pamoja na wabunge kadhaa ni baadhi ya shakhsia walioshiriki na kutoa hotuba katika kikao hicho.
Waandishi bora wanawake wa Kiislamu walitunukiwa zawadi ya kimataifa ya 'Utukufu wa Mwanadamu' ya kupambana na uzayuni duniani, mbele ya hadhara kubwa ya waandishi wa ndani na kigeni. 685028