Hayo yamesemwa na Umm Abbas al Namir, mtafiti wa masuala ya Qur'ani wa Saudi Arabia katika mahojiano yake na shirika la habari la IQNA. Ameongeza kuwa Iran ya Kiislamu ambayo ni Ummul Quraa ya ulimwengu wa Kiislamu imeweza kuwapa Waislamu uhai mpya na kueneza mafundisho ya Qur'ani baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Amesema kuwa utamaduni wa Qur'ani wa wananchi wa Iran umetokana na taathira za wafasiri wakubwa wa Qur'ani kama Allama Tabatabai na Imam Khomeini Mwenyezi Mungu awarehemu.
Umm Abbas al Namir ambaye ameshiriki katika Kongamano la Kimataifa la Watafiti wa Kike wa Qur'ani ametunukiwa zawadi ya mlinganiaji bora wa mafundisho ya Qur'ani. 684900