IQNA

Al Azhar kuanzisha kiwanda cha kuchapisha Qur'ani

16:31 - October 31, 2010
Habari ID: 2022943
Wanachama wa Baraza la Uhakiki la al Azhar waliokutana hivi karibuni chini ya uenyekiti wa Sheikh Mkuu wa al Azhar Ahmad al Tayyib wamechukuwa uamuzi wa kuanzisha kiwanda cha kuchapisha Qur'ani tukufu.
Msemaji wa Sheikh wa ala Azhar Muhammad Rafa' al Tahtawi amesema kuwa baada ya taasisi kadhaa kuchapisha nakala za Qur'ani zenye makosa ya kichapa, Baraza la Uhakiki la al Azhar lilikutana hivi majuzi na kuchunguza uwezekano wa kuanzisha kiwanda cha uchapisha wa Qur'ani kama kile cha kuchapisha Qur'ani nchini Saudi Arabia.
Mwezi uliopita baraza hilo lilivitayarisha viwanda vya uchapishaji nchini Misri kwamba iwapo vitachapisha Qur'ani zenye makosa ya kichapa vitanyang'anywa vibali.
Baraza hilo limesisitiza kuwa licha ya tahadhari hiyo baadhi ya viwanda vya uchapishaji vingali vinachapisha nakala zenye makosa za Qur'ani Tukufu. 685618

captcha