Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Idara ya Magereza ya Iran Hujjatul Islam Tahami amesema, 'mbali na wafungwa, wafanyakazi wa magereza pia wanajitahidi kuihifadhi Qur'ani Tukufu'.
Sheikh Tahami ameyasema hayo katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran baada ya kuhutubia warsha ya wahubiri wa kidini katika magereza.
Afisa huyo wa Idara ya Magereza ya Iran amesema hivi karibuni kulifanyika mashindano ya Qur'ani katika mji wa Shiraz ambapo wafungwa 330 walishiriki. Ameongeza kuwa mashindano hayo yalijumuisha kuhifadhi, kusoma na kuitafsiri Qur'ani Tukufu.
685708