IQNA

Kongamano la Kimataifa la 'Halal' kufanyika London

10:51 - November 02, 2010
Habari ID: 2023821
Kongamano la pili la kimataifa la bidhaa halali litafanyika Tarehe 10-11 Novemba mwaka huu mjini London.
Kwa mujibu wa tovuti ya Halal Focus, kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Bidhaa Halali IHI kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kiislamu wa Malaysia na vile vile mashirika kadhaa yaliyo katika sekta ya bidhaa halali. Kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Earls Court mjini London na inatazamiwa kuwa washika dau wa sekta hiyo kutoka maeneo yote duniani watashiriki.
Hivi sasa Waislamu wengi duniani na hasa bara Ulaya wanasistiza umuhimu wa kutumia bidhaa halali katika maisha yao ya kila siku. Sekta ya chakula na vinywaji imetajwa kama mojawapo ya sekta muhimu zaidi za bidhaa halali duniani.
Kati ya masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la bidhaa halali mjini London ni pamoja na suala la kuhakikisha uhalali wa bidhaa zinazotajwa kuwa halali. Aidha suala la taasisi za kusajili bidhaa halali linatazamiwa kujadiliwa.
686778
captcha