Sayyid al Muhri ametegemea hadithi ya Imam Ja'far Swadiq (as) akijibu swali kwamba je, mwanamke anaweza kwenda kuhiji Makka bila ya kuwa na maharimu wake au la? Alisema "iwapo mwanamke atakuwa na uhakika kuhusu usalama wake anaweza kwenda kuhiji bila ya kuwa na maharimu."
Sayyid Muhri amesema kuwa hii leo kuna kamati za kulinda wanawake katika misafara ya hija ambazo zinaundwa na wanawake wenye kuaminika na wanawake wamaweza kwenda hija kwa kutumia misafara hiyo.
Al Muhri amesema kuwa si sahihi kwamba mwanamke hawezi kwenda hija bila ya kuwa na maharimu.
Mwakilishi huyo wa maraji wa kidini nchini Kuwait ameongeza kuwa marajii na wanazuoni wote wa fiqhi wa Shia wamejuzisha hija ya mwanamke aliyeolewa au mshichana bila ya kuwa na maharimu. 685963