IQNA

Kongamano la kuususia utawala haramu wa Israel

11:46 - November 04, 2010
Habari ID: 2025341
Kongamano la 85 la nchi za Kiarabu la kuususia utawala haramu wa Israel limefanyika katika mji mkuu wa Syria Damascus na kuhudhuriwa na nchi 15 za Kiarabu pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Mmoja wa waandalizi wa kongamano hilo Muhammad Subeih amesema kuwa mkutano huo una nafasi muhimu katika kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel, ubaguzi wa kimbari pamoja na jinai za utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina. Amesema utawala haramu wa Israel unapaswa kususiwa kikamilifu ili kufichua utambulisho wake wa kibaguzi. Ameishukuru Syria kwa kuwa mwenyeji wa Idara ya Nchi za Kiarabu la kuususia utawala haramu wa Israel.
Naye katibu Mkuu wa Idara ya Nchi za Kiarabu la kuususia utawala haramu wa Israel amesema utawala huo ungali unaendeleza jinai zake za kinyama dhidi ya Wapalestina.
Washiriki katika kongamano hilo wamesisitiza kuwa kuususia utawala haramu wa Israel ni muhimu sasa zaidi ya wakati wowote ule.
688222

captcha