Sayyid Muhammad Hadi Ayazi Mkuu wa Idara ya Kijamii na Utamaduni katika Baraza la Jiji la Tehran amesema vyuo hivyo vitaanzishwa katika maeneo tofauti ya mji huu.
Ameongeza kuwa Baraza Kuu la Qur'ani Tukufu limebuniwa katika Baraza la Jiji ili kuratibu shughuli za Qur'ani mjini Tehran.
Amesema kuna mpango wa kujena kituo kikubwa cha Qur'ani Tukufu, kuandaa mashindano a Qur'ani na vile vile kuanzisha vyuo vya Qur'ani Tukufu kote mjini Tehran.
Afisa huyo amesema kuwa hivi sasa Baraza la Jiji la Tehran limezidisha maradufu shughuli za Qur'ani ikilinganishwa na miaka iliyopita.
687067