IQNA

Waliosilimu wafadhiliwa kufanya ibada ya hija

16:09 - November 08, 2010
Habari ID: 2027854
Jumuiya ya Kimataifa ya Waliosilimu imesema mwaka huu itawafadhili kikamilifu watu 50 waliosilimu kufanya ibada ya hija.
Jumuiya hiyo yenye makao yake nchini Saudia imesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni imewafadhili watu 400 waliosilimu kutoka nchi mbalimbali kufanya ibada ya hija.
Katika mpango wa mwaka huu, Jumuiya ya Kimataifa ya Waliosilimu imesema mbali na kuwapelekea hija watu hao 50 pia watapata fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria ya Makka na vilevile kuutembelea mji mtakatifu wa Madina.
Wakuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waliosilimu wamesema wale waliosilimu ambao wanataka kushiriki katika mpango huo wa kwenda hija wanaweza kuutembelea ukurasa wa intaneti wa www.4newmuslims.org na kujaza fomu za maombi ya kwenda kutekeleza ibada hiyo. 690889
captcha