IQNA

Zawadi za mashindano ya kimataifa ya kuchapisha Qur'ani zatolewa

17:18 - November 08, 2010
Habari ID: 2028028
Sherehe za kutoa zawadi za mashindano ya kwanza ya kimataifa ya kuchapisha Qur'ani Tukufu zimefanyika leo mjini Tehran zikihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran Sayyid Muhammad Husseini.
Sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa mukutano wa Niyavarani jijini Tehran.
Washindi wa kwanza 8 wametunukiwa zawadi ambao mmoja wao alikuwa kutoka nje ya nchi. Nafasi ya pili ilikuwa na washindi 7 na vilevile nafasi ya tatu.
Mashindano hayo yalifunguliwa jana na Hujjatul Islam Hamiid Muhammadi, Kaimu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran.
Vilevile maonyesho ya kazi na athari za mashindano ya kwanza ya kimataifa ya kuchapisha Qur'ani Tukufu yataendelea hadi tarehe 11 Novemba. 691413
captcha