IQNA

Ramani 135,000 za sehemu za kuzuru mjini Makka zasambazwa

10:59 - November 13, 2010
Habari ID: 2030500
Kamati ya Uhandisi inayofungamana na Jumuiya ya Kiarabu ya al-Kashifa ya Saudi Arabia imechapisha zaidi ya ramani 135,000 zinazohusiana na sehemu takatifu za ziara katika mji mtakatifu wa Makka kwa ajili ya kusambazwa kati ya mahujaji.
Akizungumzia suala hilo, Muqrin al-Muqarran mkuu wa vituo vya kuwahudumia mahujaji mjini Makka amesema kuwa ramani hizo zitasambazwa na vituo 17 vya mwongozo na maelezo vilivyoko Mina na Arafa. Amesema kamati iliyotajwa imetayarisha ramani hizo kwa kutegemea teknolojia ya hali ya juu ya Google Earth.
Amesema mwishoni kwamba kamati hiyo pia ina lengo la kuchapisha vijitabu 1300 kuhusiana na eneo la Arafa hadi Mina na vijitabu vingine 700 kuhusiana na Arafa ili kusambazwa miongoni mwa mahujaji. 693830
captcha