IQNA

Kuzinduliwa idara za utoaji vyeti vya bidhaa halali Malaysia

14:42 - November 14, 2010
Habari ID: 2031759
Shirika la Ustawi wa Kiislamu la Malaysia litaanzisha idara za utoaji vyeti vya bidhaa halali katika kila jimbo la nchi hiyo ili kuimarisha viwango vinavyohitajika kitaifa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Bernama Muhammad Sheikh Abdul Aziz Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo aliyekuwa akizungumza katika kikao cha 84 cha Baraza la Halmashauri za Kiislamu za Malaysia amesema kuwa uchunguzi kuhusiana na uendeshwaji wa shughuli za idara hizo ungali unaendelea na kwamba matokeo yake yatajulikana hivi karibuni. Abdul Aziz pia amesema kuwa utolewaji wa vyeti hivyo hivi sasa unawezekana kupitia mtandao wa intaneti kwa anwani ifuatayo: www.halal.gov.my. Amesema idara za utoaji vyeti hivyo zinapaswa kuanzishwa haraka iwezekanavyo katika miji yote ya Malaysia ili kukidhi mahitaji ya wateja wanaoongezeka kila siku. Amesema idara hizo zitapewa maabara ambayo yatawezesha uainishwaji wa bidhaa halali na zisizo halali na kisha kutoa vyeti kwa bidhaa zinazofaa. 694299
captcha