IQNA

Waislamu wa Ufaransa watakiwa kuondoka nchini humo

15:10 - November 14, 2010
Habari ID: 2031865
Kundi la watu wasiojulikana limetuma barua kwa msikiti wa Strasbourg nchini Ufaransa likitishia kwamba Waislamu watafukuzwa nchini humo.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa barua hiyo ambayo imetumwa kwa msikiti wa Ayyub Sultan inakipengee kinachowaambia Waislamu 'ondokeni katika nchi yetu la sivyo tutakufukuzeni sisi wenyewe'.

Msemaji wa Waislamu wa Strasbourg Yahya Nalband amesema kuhusu hatua hiyo ya kibaguzi kwamba kandokando ya barua hiyo kulikuwa na ukurasa uliochomwa moto nusu wa kitabu kitukufu cha Qur'ani. Watumaji wa barua hiyo pia wametishia kuwaua Waislamu.
Yahya Nalband amesema kuwa polisi ya Ufaransa inafanya uchunguzi wa kuwatia nguvuni watu waliohusika na kitendo hicho cha kibaguzi.
Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, msemaji wa msikiti wa Strasbourg amesema Waislamu wa Ufaransa wanalaani vikali kitendo hicho na wanaelewa kwamba kinafanyika kwa lengo la kutia tashwishi katika fikra zao. Amesisitiza juu ya kuchukuliwa hatua za kupambana na watu wanaofanya vitendo kama hivyo. 695340

captcha