Kasisi huyo mchochezi na anayekosea heshima mara kwa mara matukufu ya Kiislamu na Waislamu, mara hii amechukua hatua ya kuchekesha ya kuwataka Wakristo wakusanyike katika eneo yalipokuwa majengo pacha mjini New York katika siku ya Idul Adh'ha ili kudhihirisha malalamiko yao dhidi ya Waislamu wanaodaiwa kuwa ndio waliohusika na milipuko ya Septemba 11, 2001 katika eneo hilo. Katika matamshi mengine ya kijahili, kasisi huyo amedai kwamba Misri ni nchi ya Wakristo wa Kikopti ambayo ilitekwa nyara na kukaliwa kwa mabavu na Waislamu. Ametaka Mayahudi wawafukuze Waislamu katika mji wa Beitul Muuqaddas huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kuuteka tena kikamilifu mji huo.
Kasisi huyo mchochezi pia amewataka wakazi wa kusini mwa Sudan wafanye juhudi za kujitenga na serikali ya kaskazini na kuanzisha nchi na serikali mpya ya Kikristo katika eneo hilo. 696213