Ahmad Sharifi msimamizi wa mradi wa technohama katika Chuo cha Kidini cha Qum amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa ‘Sira ya Maasumin’, ‘Historia ya Iran’, ‘Meshkat al Anwar’, ‘Kazi zote za Allamah Hassanzadeh Amoli’, ‘Orvat-un-Nur’ na ‘Nur-ul-Faqaha’ ni kati ya programu zitakazozinduliwa katika mustakabali wa karibu.
Ameendelea kusema kuwa mbali na programu hizo , kituo hicho cha utafiti kinapanga kusambaza CD kuhusu, ‘Nahjul Balagha’, ‘Shahnameh ya Ferdowsi’, ‘Mashairi ya Hafiz’, ‘Jame-ul-Ahadith No.3’, ‘Wasail-ush-Shia’ na ‘Fiqhi ya Pamoja kwa Lugha tatu’. Ameongeza kuwa baadhi ya programu hizi za kompyuta zinaweza kutumika katika simu za mkononi.
695426