IQNA

Mashindano ya Qur'ani na Hadithi ya wanachuo wa kidini Iran

12:39 - November 18, 2010
Habari ID: 2033521
Wanachuo 9000 wa kidini kutoka mataifa 72 duniani wameshiriki katika awamu ya 16 ya Olimpiadi ya Kimataifa ya Qur'ani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (SAW) mjini Qum, Iran.
Kwa mujibu wa Muhammad Reza Saleh Mkuu wa masuala ya kiutamaduni na kielimu katika chuo hicho, amesema olimpiadi hiyo itakuwa na vitengo 56 ikiwa ni pamoja na na vitengo 40 vya mitihani ya maandishi na simulizi na vilevile vitengo 16 vitakavyohusu kazi za Qur'ani na Hadithi.
Amesema kuwa, ‘olimpiadi hiyo itakuwa na vitengo vitatu vya wanachuo, wahadhiri na familia’, na kuongozea kuwa, mchujo wa olimpiadi ya mwaka huu ulifanyika nchini Iran na katika nchi 34.
Fainali ya wanaume ya Olimpiadi itafanyika Novemba 20-21 na ile ya wanawake itafanyika Novemba 21.
‘Kwa ujumla washiriki 200 watachaguliwa kama washindi wa vitengo mbalimbali na kutunukiwa zawadi mwishoni mwa olimpiadi’.
Bw. Salehi ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (SAW) daima hufuata malengo ya Qur'ani katika shughuli zake zote za kielimu, kiutamaduni na kiutafiti.
696313

captcha