Kwa mujibu wa maelezo ya Msikiti wa Zainabiyya wa mjini Istanbul, sherehe hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Kishia ya Gunisigi Dernegi ya Igdir na imepangwa kuanza leo adhuhuri.
Umati mkubwa wa Mashia na wapenzi wa Ahlul Bait (as) unatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo. Selahattin Özgündüz, mkuu wa Jumuiya na Msikiti wa Zeinabiyya atashiriki pia katika sherehe hiyo.
Sherehe nyingine kama hiyo imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa na Muungano wa Wanazuoni wa Ahlul Bait (as) wa Uturuki katika mji huohuo wa Igdir. 697608