IQNA

Jumuiya za Kiislamu Ulaya zalaani ugaidi Iraq

14:46 - November 21, 2010
Habari ID: 2034694
Umoja wa Jumuiya za Kiislamu Barani Ulaya umelaani hujuma za kigaidi dhidi ya misikiti na makanisha nchini Iraq.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Umoja wa Jumuiya za Kiislamu Barani Ulaya umetoa taarifa na kusema, ‘mashambulio ya kigaidi nchini Iraq yanayosababisha umwagaji wa damu za raia wasio na hatia na kuvunjua heshima maeneo ya kidini ni ukiukaji wa haki’.
Taarifa hiyo imesema Wakristo wa Iraq ni sehemu ya jamii ya nchi hiyo ambao wamekuwa wakiishi nchini humo kwa muda mrefu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa Wakristo ni sehemu ya jamii za nchi za Kiarabu na Kiislamu.
Umoja wa Jumuiya za Kiislamu Barani Ulaya umesema kushambuliwa Wakristo nchini Iraq ni kosa kubwa litakalozusha matatizo katika ustaarabu wa Kiarabu na Kiislamu na kuvuruga thamani za kuishi pamoja kwa amani Mashariki ya Kati.
Umoja wa Jumuiya za Kiislamu Barani Ulaya wenye makao yake Brussels Ubelgiji unajumuisha mamia ya jumuiya za Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za Ulaya.
698335
captcha